• HABARI MPYA

  Sunday, November 12, 2023

  MANCHESTER CITY YABANWA NA CHELSEA DARAJANI, SARE 4-4


  WENYEJI, Chelsea FC wametoa sare ya kufungana mabao 4-4 na Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Chelsea leo yamefungwa na Thiago Silva dakika ya 29, Raheem Sterling dakika ya 37, Nicolas Jackson dakika ya 67 na Cole Palmer dakika ya 90 na ushei, wakati ya Manchester City yamefungwa na Erling Haaland dakika ya 25 kwa penalti na 47, Manuel Akanji dakika ya 45 na ushei, Rodri dakika ya 86.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City inafikisha pointi 28 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi moja zaidi ya zote, Liverpool na Arsenal baada ya timu zote kucheza mechi 12.
  Kwa upande wao Chelsea baada ya sare ya leo wanafikisha pointi 16 na kusogea nafasi ya 10 kufuatia kucheza mechi 12 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YABANWA NA CHELSEA DARAJANI, SARE 4-4 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top