• HABARI MPYA

  Friday, November 03, 2023

  MBEYA KWANZA NA BIASHARA ZASHINDA, FGA SARE NA COSMO CHAMPIONSHIP


  TIMU ya Mbeya Kwanza leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Cocpo United ya Mwanza katika mchezo wa Ligi ya NBC Championship Tanzania Bara Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Mechi nyingine za Championship leo, Biashara United imeichapa Mbeya City 2-1 Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza, wakati Fountain GateTalents imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Cosmopolitan Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Kwa matokeo ya leo, Mbeya Kwanza inapanda kileleni ikifikisha pointi 20 katika mchezo wa tisa, ikiizidi pointi moja Ken Gold ya Mbeya pia, ambayo pia ina mchezo mmoja mkononi - wakati Copco inabaki na pointi zake 11 nafasi ya nane baada ya kucheza mechi tisa.
  Ligi ya NBC Championship inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo minne, Green Warriors na Mbuni FC Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, Ruvu Shooting na Pamba FC Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, Ken Gold na Stand United Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya na Transit Camp dhidi ya TMA Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA KWANZA NA BIASHARA ZASHINDA, FGA SARE NA COSMO CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top