• HABARI MPYA

  Friday, November 03, 2023

  KAGERA SUGAR YAWAKANDA TANZANIA PRISONS 2-1 KAITABA


  WENYEJI, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 
  Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Obrey Chirwa kwa penalti dakika ya 20 na Cleophace Mkandala dakika ya 68, wakati bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Khamis Mcha 'Vialli' dakika ya 72.
  Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya saba, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake saba nafasi ya 14 katika ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi tisa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAWAKANDA TANZANIA PRISONS 2-1 KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top