• HABARI MPYA

  Friday, November 24, 2023

  SINGIDA BIG STARS YAWACHAPA MAJIRANI DODOMA 2-1 JAMHURI


  TIMU ya Singida Fountain Gate imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ yamefungwa na kiungo Morice Chukwu dakika ya na saba na beki Augustino Samson aliyejifunga dakika ya 13, wakati bao pekee la Dodoma Jiji limefungwa na Paul Peter Dalila ya 64.
  Kwa ushindi huo, Singida Fountain Gate wanafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya tano, wakati Dodoma Jiji wanabaki na pointi zao 15 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAWACHAPA MAJIRANI DODOMA 2-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top