• HABARI MPYA

  Wednesday, November 08, 2023

  TIMU YA NOVATUS DISMAS YAICHAPA BARCELONA 1-0 LIGI YA MABINGWA


  KIUNGO wa Kimataifa wa Tanzania, Novatus Dismas Miroshi jana alikuwa benchi muda wote timu yake, Shakhtar Donetsk ikiichapa Barcelona 1-0 katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Volksparkstadion Jijini Hamburg, Ujerumani.
  Bao pekee la Shakhtar Donetsk ya Ukraine lilifungwa na mshambuliaji Danylo Sikan dakika ya 40 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi sita, ingawa wanabaki nafasi ya tatu wakizidiwa pointi tatu na FC Porto na FC Barcelona baada ya wote kucheza mechi nne, wakati Royal Antwerp ya Ubelgiji haina pointi na inashika mkia.
  Novatus aliyejiunga na Shakhtar Donetsk Septemba 1, mwaka 2023 kwa mkataba wa mwaka mmoja hadi Juni 30 mwaka 2024, hadi sasa amecheza mechi tano, moja tu ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya FC Porto wakifungwa 3-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA NOVATUS DISMAS YAICHAPA BARCELONA 1-0 LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top