• HABARI MPYA

  Wednesday, November 22, 2023

  SIMBA SC YATAMBULISHA JEZI ZA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA


  KLABU ya Simba imetambulisha jezi zake maalum itakazotumia katika Ligi ya Mabingwa Afrika kuelekea mchezo wao wa kwanza wa Kundi B dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast Jumamosi Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Wachezaji wa Simba waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ni kipa Aishi Manula na mshambuliaji Kibu Dennis ambao wameungana na wenzao mazoezini Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam.
  Aidha, kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza aliyekuwa kwenye kikosi cha Burundi ambacho kinachezea mechi zake hapa Dar es Salaam pia leo ameingia kambini – na sasa wanasubiriwa beki Henock Inonga Baka ‘Varane’ aliyekuwa DRC na kiungo Clatous Chotta Chama wa Zambia warejee kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATAMBULISHA JEZI ZA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top