• HABARI MPYA

  Saturday, November 11, 2023

  ARSENAL YAWAKANDA BURNLEY 3-1 NA KURUDI KWENYE ‘ANGA ZA UBINGWA’


  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Leandro Trossard dakika ya 45 na ushei, William Saliba dakika ya 57 na Oleksandr Zinchenko dakika ya 74, wakati la kufuatia machozi la Burnley limefungwa na Josh Brownhill dakika ya 54.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Manchester City ambao wamecheza mechi 11, wakati Burnley inabaki na pointi zake nne za mechi 12 nafasi ya 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAWAKANDA BURNLEY 3-1 NA KURUDI KWENYE ‘ANGA ZA UBINGWA’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top