• HABARI MPYA

  Wednesday, November 01, 2023

  SINGIDA BIG STARS YAAMBULIA SARE KWA IHEFU SC 2-2 LITI


  WENYEJI, Singida Big Stars wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mabao yote ya Singida Big Stars yamefungwa na Habib Haji Kyombo dakika ya 31 na 40, wakati ya Ihefu SC yamefungwa na Ismail Mgunda dakika ya 26 na Jaffary Kibaya dakika ya 70.
  Kwa matokeo hayo Singida Big Stars inafikisha pointi tisa na kusogea nafasi ya tisa, wakati Ihefu SC inafikisha pointi nane na kusogea nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi nane
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAAMBULIA SARE KWA IHEFU SC 2-2 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top