// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); IBRAHIM BACCA AJITIA KITANZI JANGWANI HADI 2027 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE IBRAHIM BACCA AJITIA KITANZI JANGWANI HADI 2027 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, November 29, 2023

  IBRAHIM BACCA AJITIA KITANZI JANGWANI HADI 2027


  BEKI wa kati, Ibrahim Abdallah Hamad 'Bacca' ameongeza mkataba wa kuendelea na kazi katika klabu ya Yanga hadi mwaka 2027.
  Bacca (26) aliyejiunga na Yanga Januari 14, mwaka jana akitokea KMKM ya Zanzibar anapewa mkataba mpya baada ya kazi nzuri aliyofanya mwaka mmoja akiwa timu ya Wananchi.
  Sambamba na kumuongeza mkataba, Yanga imempa heshima Bacca kwa kuifanya mechi yake ya pili ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam iwe siku maalum ya mlinzi huyo hodari, yaani 'Bacca Day'.
  Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) kila moja zimdhamini Bacca Day kwa dau la Sh. Milioni 20, maana yake Yanga imetengeneza Sh. Milioni 40 tukio maalum la mchezaji huyo. 
  Ikumbukwe Yanga ilianza mechi zake za Kundi D kwa kuchapwa 3-0 na wenyeji, CR Belouizdad Ijumaa Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria, huku Al Ahly wakiichapa Medeama ya Ghana 3-0 Uwanja wa Al Salam Jijini Cairo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IBRAHIM BACCA AJITIA KITANZI JANGWANI HADI 2027 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top