• HABARI MPYA

  Saturday, November 25, 2023

  MAN CITY NA LIVERPOOL NGOMA DROO 1-1 ETIHAD


  MABINGWA watetezi, Manchester City leo wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mshambuliaji wa Kimataifa wa Norway, Erling Haaland alianza kuifungia Manchester City dakika ya 27 akimalizia kazi nzuri ya beki Mholanzi, Nathan Benjamin Aké, kabla ya beki Muingereza, Trent John Alexander-Arnold kuisawazishia Liverpool dakika ya 80 akimalizia pigo la mshambuliaji Mmisri, Mohamed Salah.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City wanafikisha pointi 29 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi moja zaidi ya Liverpool inayofuatia nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY NA LIVERPOOL NGOMA DROO 1-1 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top