TIMU ya Azam FC imezinduka na kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na viungo Muivory Coast, Kipre Junior dakika ya 52, Mguinea Gibrill Sillah dakika ya 70 mshambuliaji Msenegal, Alassane Diao dakika ya 73.
Ushindi huo unaokuja baada ya vipigo viwili kutoka Yanga 3-2 na Namungo FC 3-1 unaifanya Azam FC ifikishe pointi 16 na kurejea nafasi ya tatu, wakati Mashujaa inabaki na pointi zake nane na kushukia nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi nane.
0 comments:
Post a Comment