• HABARI MPYA

  Saturday, November 25, 2023

  NEWCASTLE UNITED YAITANDIKA CHELSEA 4-1


  WENYEJI, Newcastle United leo wameitandika Chelsea FC mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. James' Park mjini Newcastle upon Tyne.
  Mabao ya Newcastle United yamefungwa Alexander Isak dakika ya 13, Nahodha Jamaal Lascelles dakika ya 60, Joelinton dakika ya 61 na Anthony Gordon dakika ya 83, wakati bao pekee la Chelsea limefungwa na Raheem Sterling dakika ya 23.
  Chelsea ilimaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Reece James kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 73.
  Kwa ushindi huo, Newcastle United wanafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya sita, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 16 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 13. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEWCASTLE UNITED YAITANDIKA CHELSEA 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top