• HABARI MPYA

  Wednesday, November 08, 2023

  YANGA YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAITWANGA COASTAL 1-0 MKWAKWANI


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameendeleza shangwe kwa mashabiki wao baada ya kuichapa Coastal Unión bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Bao pekee la Yanga katika mchezo wa leo limefungwa na mshambuliaji Clement John Mzize dakika ya 71 kwa kichwa akimalizia krosi ya winga Mkongo, Jesús Moloko kutoka upande wa kulia.
  Wahusika wote wa bao hilo walitokea benchi, Mzize ya mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda dakika ya 59 na Moloko akimrithi Mudathir Yahya dakika ya 70.
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 24 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya Azam FC inayofuatia baada ya wote kucheza mechi tisa, wakati Coastal Unión inabaki na pointi zake saba za mechi tisa nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAITWANGA COASTAL 1-0 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top