• HABARI MPYA

  Thursday, November 16, 2023

  ZANZIBAR MABINGWA CECAFA U15, BARA WASHINDI WA TATU


  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ya Zanzíbar leo imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U15) baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya wenyeji, Uganda kufuatia sare ya 1-1 mjini Kampala.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Njeru mjini Kampala nchini Uganda, mabao yote yalipatikana kipindi cha kwanza wenyeji wakitangulia kabla ya Karume Boys kusawazisha.
  Kwa upande wao, Tanzania Bara wamefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo uliotangulia hapo hapo Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha FUFA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZANZIBAR MABINGWA CECAFA U15, BARA WASHINDI WA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top