• HABARI MPYA

  Monday, November 27, 2023

  KAGERE AFUNGA, SINGIDA YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 LITI


  WENYEJI, Singida Fountain Gate wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Unión katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mabao ya Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ yamefungwa na mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere dakika ya 30 na beki Mkongo Felly Mulumba aliyejifunga dakika ya 52, wakati bao pekee la Coastal Unión limefungwa na mshambuliaji Maabad Maulid dakika ya 72.
  Kwa ushindi huo, Singida Fountain Gate inafikisha pointi 18 na kusogea nafasi ya nne, wakati Coastal Unión inabaki na pointi zake 10 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERE AFUNGA, SINGIDA YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top