• HABARI MPYA

  Wednesday, November 29, 2023

  NA HIVI NDIVYO BENCHIKA ALIVYOANZA KAZI SIMBA SC


  BAADA ya kutambulishwa rasmi jana, Kocha mpya Mkuu wa Simba SC, Mualgeria Abdelhak Benchikha leo ameanza kukinoa kikosi hicho Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam.
  Simba SC inajiandaa na mchezo wake wa pili Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, wa Jwaneng Galaxy Jumamosi Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana.
  Ikumbukwe mechi ya kwanza ya Kundi B Ligi ya Mabingwa, Simba ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
  Wakati Benchika anatambulishwa jana aliahidi kurejesha furaha kwa mashabiki wa Simba iliyopotea baada ya timu kwenda mechi tatu mfululizo bila ushindi tangu ifungwe 5-1 na Yanga Novemba 5, ikadroo 1-1 mfululizo, na Namungo FC na ASEC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NA HIVI NDIVYO BENCHIKA ALIVYOANZA KAZI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top