• HABARI MPYA

  Thursday, November 30, 2023

  BENCHIKA AWAACHA AISHI, BOCCO NA CHILUNDA SAFARI YA BOTSWANA


  KOCHA mpya Mkuu wa Simba SC, Mualgeria Abdelhak Benchika amewaacha kipa Aishi Manula na washambuliaji, Nahodha John Bocco na Shaaban Iddi Chilunda katika safari ya Botswana kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy Jumamosi.
  Aishi ameachwa kwa sababu aliumia akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa wiki iliyopita, lakini Bocco na Chilunda hawapo kwenye mpango wa Benchika katika mechi yake ya kwanza kazini Simba SC.
  Simba SC unaondoka Alfajiri ya kesho kwenda Francistown  kwa ajili ya mchezo wake huo wa pili wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Ikumbukwe mechi ya kwanza ya Kundi B Ligi ya Mabingwa, Simba ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENCHIKA AWAACHA AISHI, BOCCO NA CHILUNDA SAFARI YA BOTSWANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top