• HABARI MPYA

  Friday, November 24, 2023

  AZAM FC YAITANDIKA MTIBWA SUGAR 5-0 KIPRE APIGA HAT TRICK


  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo mshambuliaji Muivory Coast, Kipre Junior matatu dakika za 29,43 na 63 na beki Lusajo Mwaikenda dakika ya 61 na kiungo Feisal Salum dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 10 ingawa inabaki nafasi ya pili kwa kuzidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Mtibwa Sugar baada ya kichapo cha leo wanaendelea kushika mkia katika Ligi ya timu 16 wakibaki na pointi zao tano baada ya kucheza pia mechi 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAITANDIKA MTIBWA SUGAR 5-0 KIPRE APIGA HAT TRICK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top