• HABARI MPYA

  Wednesday, November 29, 2023

  BARA YAKWAA KISIKI KWA SUDAN KUSINI CECAFA U18


  TANZANIA Bara imekwaa kisiki baada ya kuchapwa 2-1 na Sudan Kusini katika mchezo wa Kundi B michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 18 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U18) asubuhi ya leo Uwanja wa Kakamega nchini Kenya.
  Matokeo hayo yanazifanya timu tatu zifungane kwa pointi kwenye kundi hilo, Zanzíbar, Sudan Kusini na Tanzania Bara ambazo kila moja ina pointi tatu, wakati Uganda ambayo haina pointi inashika mkia.
  Bara inayofundishwa na Kocha Habib Kondo itakamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na ndugu zao, Zanzíbar Jumamosi kuwania kuingia Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARA YAKWAA KISIKI KWA SUDAN KUSINI CECAFA U18 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top