• HABARI MPYA

  Thursday, November 30, 2023

  TWIGA STARS YATANGULIZA MGUU MMOJA WAFCON 2024


  TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Togo katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili na ya mwisho ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) 2024 leo Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
  Mabao ya Twiga Stars yamefungwa na mshambuliaji wa Besiktas ya Uturuki, Opa Clement mawili, dakika ya 45 na ushei kwa penalti na dakika ya 81, huku lingine Yawa Konou wa Togo akijifunga dakika ya 57.
  Timu hizo zitarudiana Desemba 5 Uwanja wa Kégué Jijini Lomé na mshindi wa jumla atakuwa amejikatia tiketi ya WAFCON ya Morocco mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS YATANGULIZA MGUU MMOJA WAFCON 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top