• HABARI MPYA

  Thursday, November 23, 2023

  NAMUNGO FC YAICHAPA IHEFU 2-0 RUANGWA MABAO YA BUSWITA NA MAJIMENGI


  WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Mabao ya Namungo FC leo yamefungwa na kiungo Pius Buswita dakika ya 36 na mshambuliaji Hamad Majimengi dakika ya 76.
  Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Ihefu SC inabaki na pointi zake nane nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAICHAPA IHEFU 2-0 RUANGWA MABAO YA BUSWITA NA MAJIMENGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top