• HABARI MPYA

  Monday, November 06, 2023

  SINGIDA BIG STARS YATANDIKA MASHUJAA FC 3-1 KIGOMA


  TIMU ya Singida Big Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Mabao ya Singida Big Stars yamefungwa na Gardiel Michael dakika ya 18, Marouf Tchakei dakika ya 44 na Habib Kyombo dakika ya 64, wakati bao pekee la Mashujaa FC limefungwa na Adam Adam dakika ya 85.
  Kwa ushindi huo Singida Big Stars inafikisha pointi 12 katika mchezo wa tisa na kusogea nafasi ya saba, wakati Mashujaa FC wanabaki na pointi zao nane za mechi nane nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YATANDIKA MASHUJAA FC 3-1 KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top