• HABARI MPYA

  Thursday, November 30, 2023

  ARSENAL YAICHAPA LENS 6-0 LIGI YA MABINGWA


  WENYEJI, Arsenal wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Lena ya Ufaransa usiku wa Jumatano Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Kai Havertz dakika ya 13, Gabriel Jesus dakika ya 21, Bukayo Saka dakika ya 23, Gabriel Martinelli dakika ya 27, Martin Odegaard dakika ya 45 na ushei na Jorginho kwa penalti dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 12 na kuendelea kuongoza Kundi B, ikifuatiwa na PSV Eindhoven ya Uholanzi pointi nane, Lena tano na Sevilla ya Hispania pointi mbili baada ya wote kucheza mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA LENS 6-0 LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top