• HABARI MPYA

  Saturday, November 25, 2023

  ARSENAL YAICHAPA BRENTFORD 1-0 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND


  BAO la kiungo wa Kimataifa wa Ujerumani, Kai Lukas Havertz dakika ya 89 limetosha kuirejesha Arsenal kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Gtech Community mjiji Brentford, Middlesex. 
  Kai Havertz aliyejiunga na Arsenal msimu huu akitokea Chelsea iliyomsajili mwaka 2020 kutoka Bayer Leverkusen ya kwao, alifunga bao hilo kwa ustadi mkubwa akimalizia kazi nzuri ya winga Muingereza mwenye asili ya Nigeria, Bukayo Ayoyinka Temidayo Saka.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 30 na kupanda juu ya msimamo wa Ligi Kuu ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 13.
  Kwa upande wao, Brentford wanabaki na pointi 16 nafasi ya 11 baada ya wao pia kucheza mechi 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA BRENTFORD 1-0 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top