• HABARI MPYA

  Thursday, November 09, 2023

  SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA NAMUNGO 1-1 UHURU


  WENYEJI, Simba SC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Namungo FC walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake tegemeo, Relliants Lusajo dakika ya 29, kabla ya mshambuliaji Mkongo, Jean Othos Baleke kuisawazishia Simba SC dakika ya 75.
  Kwa sare hiyo, Simba SC inafikisha pointi 19 katika mchezo wa nane, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi - wote wakiwa nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 24 za mechi tisa.
  Kwa upande wao, Namungo FC baada ya sare ya leo wanafikisha pointi nane baada ya kushuka dimbani Nara tisa na wanasogea nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA NAMUNGO 1-1 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top