• HABARI MPYA

  Wednesday, November 29, 2023

  BENCHIKA AKUTANA NA WACHEZAJI TAYARI KUANZA KAZI SIMBA SC


  BAADA ya kutambulishwa rasmi jana, Kocha mpya Mkuu wa Simba SC, Mualgeria Abdelhak Benchikha leo amekutana na wachezaji na kuzungumza nao kwmbini Mbweni Jijini Dar es Salaam.
  Benchika anatarajiwa kuanza kukinoa kikosi cha Simba kuelekea mchezo wake wa pili Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, wa Jwaneng Galaxy Jumamosi Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana.
  Ikumbukwe mechi ya kwanza ya Kundi B Ligi ya Mabingwa, Simba ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
  Na kama utakumbuka jana wakati Benchika anatambulishwa aliahidi kurejesha furaha kwa mashabiki wa Simba iliyopotea baada ya timu kwenda mechi tatu mfululizo bila ushindi tangu ifungwe 5-1 na Yanga Novemba 5, ikadroo 1-1 mfululizo, na Namungo FC na ASEC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENCHIKA AKUTANA NA WACHEZAJI TAYARI KUANZA KAZI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top