• HABARI MPYA

  Saturday, November 18, 2023

  MAPRO WATANO WAITWA KUIPIGANIA TWIGA STARS TIKETI YA WAFCON 2024


  KOCHA Bakari Shime ameita wachezaji watano wanaocheza timu mbalimbali Ulaya, Amerika na Asía kuunda kikosi cha timu ya taifa ya wanawake kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya pili na ya mwisho kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake Jumatano ijayo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Hao ni beki Julieath Singano anayecheza Juarez ya Mexico, viungo Enekia Kasonga wa Eastern Flames ya Saudi Arabia na Diana Lucas wa Ameds FK ya Uturuki na washambuliaji, Opa Clement wa Besiktas ya Uturuki pia na Aisha Masaka wa BK Hancken ya Sweden.
  Kwa kiasi kikubwa kikosi cha Twiga Stars kinaundwa na nyota wa klabu bingwa ya Tanzania na Afrika Mashariki na Katí, JKT Queens pamoja na wawili wa Simba Queens na mmoja wa Yanga Princess.
  Timu hizo zitarudiana mapema Desemba Uwanja wa Kégué Jijini Lomé na mshindi wa jumla atafuzu Fainali za WAFCON mwakani zitakazofanyika nchini Morocco.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAPRO WATANO WAITWA KUIPIGANIA TWIGA STARS TIKETI YA WAFCON 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top