• HABARI MPYA

  Friday, November 03, 2023

  DODOMA JIJI YAILAZA KMC 2-1 UWANJA WA UHURU


  WENYEJI, KMC wamechapwa mabao 2-1 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Zidane Sereri dakika ya tatu na Emmanuel Martin dakika ya 22, wakati la KMC limefungwa na Rashid Chambo dakika ya 32.
  Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya nne ikiizidi wastani wa mabao KMC baada ya wote kucheza mechi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAILAZA KMC 2-1 UWANJA WA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top