• HABARI MPYA

  Monday, November 06, 2023

  JKT QUEENS YACHAPWA 2-0 NA MAMELODI LIGI YA MABINGWA WANAWAKE AFRIKA


  TIMU ya JKT Queens jana ilianza vibaya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katka mchezo wa Kundi A Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo nchini Ivory Coast. 
  Mabao yaliyowazamisha mabingwa wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati, JKT Queens yalifungwa na kiungo wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Ester Lebohang Ramalepe dakika ya 41 na mshambuliaji wa Kimataifa wa Botswana, Tebogo Refilwe Tholakele dakika ya 75.
  Mchezo uliotangulia, wenyeji Athlético Abidjan walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Sporting Casablanca ya Morocco - na leo ni mechi za Kundi B, mabingwa watetezi, FAR Rabat na Ampem Darkoa ya Ghana Saa 2:00 usiku na Huracanes ya Equatorial Guinea dhidi ya Mandé ya Mali Saa 5:00 usiku Uwnaja wa Laurent Pokou, San-Pedro.
  JKT Queens watarudi dimbani Jumatano Saa 2:00 usiku kumenyana na wenyeji, Athlético Abidjan wakati mabingwa wa COSAFA, Mamelodi Sundowns watapambana na Sporting Casablanca. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT QUEENS YACHAPWA 2-0 NA MAMELODI LIGI YA MABINGWA WANAWAKE AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top