• HABARI MPYA

  Thursday, November 09, 2023

  ARSENAL YAPOZA MACHUNGU, YAICHAPA SEVILLA 2-0 ULAYA


  KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta jana alikuwa mwenye furaha baada ya timu yake kuweka kando machungu ya kichapo cha 1-0 kutoka Newcastle United Jumamosi katika Ligi Kuu ya England na kuilaza Sevilla 2-0.
  Mabao ya Arsenal jana yamefungwa Leandro Trossard dakika ya 29 na Bukayo Saka dakika ya 64 Uwanja wa Emirates Jijini London kwenye mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Matokeo hayo yanaiweka Arsenal kileleni mwa Kundi B ikiwa na pointi tisa, ikifuatiwa naPSV na Lens zenye pointi tano kila moja, wakati Sevilla inaendelea kushika mkiani baada ya wote kucheza mechi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPOZA MACHUNGU, YAICHAPA SEVILLA 2-0 ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top