• HABARI MPYA

  Monday, November 20, 2023

  MAMELODI MALKIA WA LIGI YA MABINGWA WANAWAKE


  TIMU ya Mamelodi Sundowns imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake baada ya kuifunga SC Casablanca ya Morocco mabao 3-0 katika mchezo wa Fainali jana Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo nchini Ivory Ivory Coast.
  Mabao ya mabinti hao wa Afrika Kusini yamefungwa na Tholakele Refilwe mawili, dakika ya 21 kwa penalti na 78 akimalizia pasi ya Melinda Kgadiete na lingine, Boitumelo Rabale dakika ya 24.
  Huo ulikuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo baada ya Mamelodi Sundowns kuichapa SC Casablanca 1-0 katika mechi ya Kundi A.
  Kwa kutwaa taji hili kwa mara ya pili kihistoria kwao, Mamelodi wamezawadiwa dola za Kimarekani 400,000, huku washindi wa pili SC Casablanca wakiondoka na dola 250,000 kwa kumaliza nafasi ya pili.
  Waliokuwa mabingwa watetezi, AS FAR ambao walimaliza nafasi ya tatu baada ya kuifunga Ampem Darkoa ya Ghana mabao 2-0 kwa pamoja wamezawadiwa dola 200,000.
  Timu za AS Mande ya Mali na JKT Queens ya Tanzania kila moja imepata dola 150,000 kwa kumaliza nafasi ya tatu kwenye makundi yao, wakati Athlético F.C. d'Abidjan ya Ivory Coast na Huracanes ya Equatorial Guinea zimepata dola 100,000 baada ya kushika mkia kundini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMELODI MALKIA WA LIGI YA MABINGWA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top