• HABARI MPYA

  Tuesday, November 21, 2023

  PRISONS YAACHANA NA KOCHA MINZIRO, TIMU APEWA MTUPA


  KLABU ya Tanzania Prisons imeachana na Kocha wake, Freddy Felix Minziro kutokana na mwenendo mbaya wa timu katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  Taarifa ya Tanzania Prisons leo imesema kwamba baada ya kuachana na Minziro aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja Julai 14 mwaka huu sasa timu itakuwa chini aliyekuwa Msaidizi wake, Shaaban Mtupa.
  Baada ya mechi tisa za awali, Tanzania Prisons imevuna pointi saba tu ikiwa inashika nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kwenye mchujo wa kuwania kubaki.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAACHANA NA KOCHA MINZIRO, TIMU APEWA MTUPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top