• HABARI MPYA

  Friday, November 03, 2023

  MTIBWA SUGAR WACHAPWA 2-1 NA JKT TANZANIA MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wamechapwa mabao 2-1 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Danny Lyanga dakika ya 22 na Najim Magulu dakika ya 87, wakati la Mtibwa Sugar limefungwa na Juma Nyangi dakika ya 45.
  Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi sita, ingawa wanabaki nafasi ya sita, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake tano mkiani baada ya wote kucheza mechi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WACHAPWA 2-1 NA JKT TANZANIA MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top