// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA YAZINDUA BACCA DAY MECHI DHIDI YA AL AHLY JUMAMOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA YAZINDUA BACCA DAY MECHI DHIDI YA AL AHLY JUMAMOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Monday, November 27, 2023

  YANGA YAZINDUA BACCA DAY MECHI DHIDI YA AL AHLY JUMAMOSI


  KLABU ya Yanga imesema mechi yao ya pili ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam itakuwa siku maalum ya beki wake,Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na itaitwa Bacca Day.
  Yanga imezindua ‘Bacca Day’ leo visiwani Zanzibar sambamba na kutangaza rasmi mwanzo wa hamasa za kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Ahly. 
  Na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) kila moja imejitolea kudhamini shughuli hiyo kiwa dau la Sh. Milioni 20, maana yake kwa wiki hii moja Yanga imetengeneza Sh. Milioni 40 kwenye Bacca Day.
  Ikumbukwe Yanga ilianza mechi zake za Kundi D kwa kuchapwa 3-0 na wenyeji, CR Belouizdad Ijumaa Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria, huku Al Ahly wakiichapa Medeama ya Ghana 3-0 Uwanja wa Al Salam Jijini Cairo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAZINDUA BACCA DAY MECHI DHIDI YA AL AHLY JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top