• HABARI MPYA

        Sunday, November 05, 2023

        LUIS DIAZ AINUSURU LIVERPOOL KUPIGWA NA LUTON TOWN


        WENYEJI, Luton Town wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Kenilworth Road mjini Luton, Bedfordshire.
        Tahith Chong alianza kuifungia Luton Town dakika ya 80, kabla ya Luis Diaz kutokea benchi na kuisawazishia Liverpool dakika ya 90 na ushei.
        Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 24 na kusogea nafasi ya tatu, wakati Luton Town imefikisha pointi sita na kusogea nafasi ya 17 baada ya wote kucheza mechi 11.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: LUIS DIAZ AINUSURU LIVERPOOL KUPIGWA NA LUTON TOWN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry