• HABARI MPYA

    Monday, November 27, 2023

    KIKAO CHA BODI NA WACHEZAJI SIMBA SC CHAAMUA; "SHUGHULI INAANZA"


    BODI ya Wakurugenzi ya Simba jana ilikutana na wachezaji kambini Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kujadiliana baada ya timu kwenda mechi tatu bila ya ushindi na baada yah apo wakatoka na kauli moja kwamba; “Sasa shughuli ndiyo inaanza”.
    VIDEO: BEKI MOHAMED HUSSEIN 'TSHABALALA' AKIZUNGUMZA
    VIDEO: KIUNGO CLATOUS CHAMA AKIZUNGUMZA
    VIDEO: MSHAMBULIAJI KIBU DENNIS AKIZUNGUMZA
    Baada ya kufungwa 5-1 na Yanga Novemba 5, Simba ilidroo 1-1 mara mbili mfululizo – na Namungo hizo zote zikiwa mechi za Ligi Kuu na ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mechi ya Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo zote zilichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Mchezo ujao Simba itakuwa mgeni wa Jwaneng Galaxy Jumamosi Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana mechi ya Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika.  

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIKAO CHA BODI NA WACHEZAJI SIMBA SC CHAAMUA; "SHUGHULI INAANZA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top