• HABARI MPYA

  Thursday, November 02, 2023

  MAN UNITED YATEMESHWA CARABAO CUP KWA KICHAPO CHA 3-0


  MABINGWA watetezi, Manchester United wametolewa kwenye Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Newcastle United katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora usiku wa Jumatano Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao yaliyoipeleka Newcastle United Robo Fainali yamefungwa na Miguel Almiron dakika ya 28, Lewis Hill dakika ya 36 na Joe Willock dakika ya 60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATEMESHWA CARABAO CUP KWA KICHAPO CHA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top