• HABARI MPYA

  Thursday, November 16, 2023

  TANZANITE WALIVYOONDOKA LEO KUIFUATA NIGERIA MECHI JUMAMOSI ABUJA


  TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imeondoka leo Jijini Dar es Salaam kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano na wenyeji Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Colombia Jumapili Uwanja wa Taifa wa Moshood Abiola Jijini Abuja.
  Tanzanite inahitaji ushindi wa ugenini au sare ya kuanzia mabao 2-2 kufuatia kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.
  Katika mchezo mkali na wa kusisimua uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Nigeria ilitangulia kwa bao la Chioma Oliseh dakika ya 57, kabla ya Asnath Ubamba kuisawazishia Tanzanite dakika ya 70.
  PICHA: TANZANITE WALIVYOONDOKA DAR KUIFUATA NIGERIA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE WALIVYOONDOKA LEO KUIFUATA NIGERIA MECHI JUMAMOSI ABUJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top