• HABARI MPYA

  Tuesday, November 28, 2023

  RAIS HERSI AZINDUA TAWI LA WANA YANGA WASIOONA LEO DAR


  RAIS wa Yanga, Hersi Ally Said leo amezindua tawi la wanachama wa Yanga Wasiiona Jijini Dares Salaam.
  Akizungumza baada ya kuzindua tawi hilo la Chama cha Wasioona Tanzania (TAB), Hersi amesema kwamba ni baraka kwa klabu kuungwa mkono na ndugu zao hao wasioona na amewahakikishia atakuwa mlezi wa tawo hili siku zote.
  “Nimefarijika sana kama Rais wa hii klabu kuzindua tawi la kihistoria kwenye tasnia hii ya michezo, ni baraka kwa klabu kuungwa mkono na ndugu zetu hawa wasio ona, nawahakikishia nitakuwa mlezi wa tawi hili siku zote, asanteni sana na Mungu azidi kuwa jaalia kila lenye heri,” amesema Hersi.
  Hesrsi amezindua tawi hilo kuelekea mchezo wa pili wa Yanga katika Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Ikumbukwe Yanga ilianza mechi zake za Kundi D kwa kuchapwa 3-0 na wenyeji, CR Belouizdad Ijumaa Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria, huku Al Ahly wakiichapa Medeama ya Ghana 3-0 Uwanja wa Al Salam Jijini Cairo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS HERSI AZINDUA TAWI LA WANA YANGA WASIOONA LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top