• HABARI MPYA

  Thursday, November 09, 2023

  MAN UNITED YAJIWEKA PAGUMU LIGI YA MABINGWA ULAYA


  MATUMAINI ya Manchester United kwenda hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya jana yalizidi kufifia baada ya kuchapwa mabao 4-3 na wenyeji, FC Copenhagen katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Parken Jijini Copenhagen nchini Denmark.
  Mabao ya FC Copenhagen yalifungwa na Mohamed Elyounoussi dakika ya 45, Diogo Gonçalves kwa penalti dakika ya 45, Lukas Lerager dakika ya 83 na Roony Bardghji dakika ya 87, wakati ya Manchester United yalifungwa na mshambuliaji Mdenmark, Rasmus Hojlund mawili, dakika ya tatu na 28 na Bruno Fernandes kwa penalti dakika ya 69.
  Manchester United ilimaliza pungufu mchezo huo kufuatia Marcus Rashford kutolewa kwa nyekundu dakika ya 42 kwa kumchezea rafu mshambuliaji wa Copenhagen.
  Msimamo wa Kundi A sasa ni Bayern Munich inaongoza kwa ponti zake 12, ikifuatiwa na FC Copenhagen na Galatasaray zenye pointi nne kila moja, wakati Manchester United inayobaki na pointi zake tatu baada ya wote kucheza nne inashika mkia.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAJIWEKA PAGUMU LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top