• HABARI MPYA

  Sunday, November 12, 2023

  SALAH APIGA MBILI LIVERPOOL YAICHAPA BRENTFORD 3-0 ANFIELD


  NYOTA wa Misri, Mohamed Salah amefunga mabao mawili kuisaidia Liverpool kuichapa Brentford 3-0
  katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Salah alifunga mabao yake dakika za 39 na 62, kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Ureno, Diogo Jota kukamilisha la tatu dakika ya 74.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 27 na kusogea nafasi ya pili ikiizidi wastani wa mabao Arsenal na wote wapo nyuma ya Manchester City, wakati Brentford inabaki na pointi zake 16 za mechi 12 pia nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH APIGA MBILI LIVERPOOL YAICHAPA BRENTFORD 3-0 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top