• HABARI MPYA

    Sunday, November 26, 2023

    JKT TANZANIA YAAMBULIA SARE KWA IHEFU SC 1-1 CHAMAZI


    TIMU ya JKT Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Kiungo Said Hamisi Ndemla alianza kuifungia JKT Tanzania dakika ya 14, kabla ya mshambuliaji Ismail Mgunda kuisawazishia Ihefu SC dakika mbili baadaye.
    Kwa sare hiyo, JKT Tanzania inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya saba, wakati Ihefu SC imetimiza pointi tisa katika nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 11.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT TANZANIA YAAMBULIA SARE KWA IHEFU SC 1-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top