• HABARI MPYA

  Thursday, April 20, 2023

  KENNY MKAPA AKIMDHIBITI GEORGE LUCAS SIMBA NA YANGA 1993

   

  KIUNGO wa Simba SC, George Lucas ‘Gazza’ akitafuta maarifa ya kumpita beki wa Yanga SC, Kenneth Pius Mkapa katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (sasa Ligi Kuu) Machi 27, mwaka 1993 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) Jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-1 mabao yake yakifungwa na Said Nassor Mwamba ‘Kizota’ marehemu yote dakika ya 47 na 57 kwa pasi za Zamoyoni Mogella, wakati la watani wao lilifungwa na Edward Chumila dakika ya 75.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KENNY MKAPA AKIMDHIBITI GEORGE LUCAS SIMBA NA YANGA 1993 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top