• HABARI MPYA

  Friday, April 21, 2023

  POLISI TANZANIA YATOKA NYUMA KUICHAPA IHEFU 2-1 MOSHI


  WENYEJI, Polisi Tanzania wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Ihefu SC walitangulia kwa bao la Adam Adam dakika ya 48, kabla ya Kelvin Kongwe Sabato kuisawazishia Polisi dakika ya 62 na kufunga la ushindi dakika ya 73.
  Kwa ushindi huo, Polisi Tanzania inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 27 na kusogea nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16, wakati Ihefu inabaki na pointi zake 33 za mechi 27 pia nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YATOKA NYUMA KUICHAPA IHEFU 2-1 MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top