• HABARI MPYA

    Saturday, April 15, 2023

    TSHABALALA: SIMBA SC BADO TUPO KWENYE MBIO ZA UBINGWA


    NAHODHA Msaidizi wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala' amesema kwamba bado wapo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, hivyo mchezo dhidi ya watani wa jadi, Yanga SVC ni muhimu kushinda kesho ili kujiweka sawa.
    Simba SC watamenyana na Yanga kesho katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuanzia Saa 1:00 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Kwa upande wake, kiungo wa Yanga Mudathir Yahya Abbas amesema wao kama wachezaji wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo.
    Kwa upande wake, kocha Mbrazil wa Simba, Robert Oliveira ‘Robertinho’ amesema Simba haiwezi kubadili chochote kwenye mchezo huo, bali wataingia na mkakati maalum wa ushindi.
    Kocha Msaidizi wa Yanga, Mrundi Cedric Kaze amesema mechi ya kesho ni ya wapinzani na kila upande una motisha yake, hivyo kwa upande wao wamejiandaa kwa utulivu na wako vizuri kuelekea mchezo huo.
    Kwa sasa Yanga inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 68, ikifuatiwa na Simba yenye pointi 60 baada ya wote kucheza mechi 25 kuelekea mechi tano za mwisho za msimu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TSHABALALA: SIMBA SC BADO TUPO KWENYE MBIO ZA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top