• HABARI MPYA

  Wednesday, April 26, 2023

  SIMBA SC WALIPOTUA DAR KIBABE BAADA YA KUSHINDA 5-0 ZAMBIA 1979

   

  WACHEZAJI wa Simba SC kuanzia chini kwenda juu, kipa Athumani Mambosasa (sasa marehemu), George ‘Best’ Kulagwa, Abbas Kuka, Saad Ally, Hussein Tindwa (sasa marehemu) na Hamisi Askari (marehemu pia) wakiteremka kwenye ndege baada ya kuwasili kutoka Zambia ambako waliwafunga wenyeji, Mufurila Wanderers 5-0 katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1979. 
  Simba SC ikafuzu kwa ushindi wa jumla wa 5-4 kufuatia kufungwa 4-0 na Mufurila Wanderers Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) Dar es Salaam. Safari ya Simba iliishia raundi ya Pili ambako ilitolewa na Raccah Rovers, ikitoa sare ya 0-0 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-0 Nigeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WALIPOTUA DAR KIBABE BAADA YA KUSHINDA 5-0 ZAMBIA 1979 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top