• HABARI MPYA

  Sunday, April 23, 2023

  MAYELE APIGA ZOTE MBILI YANGA YAICHAPA RIVERS 2-0 UYO


  MABAO ya mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele kipindi cha pili yameipa Yanga ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Rivers United katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Venue Godswill Akpabio International mjini Uyo, Nigeria.
  Mayele alifunga bao la kwanza dakika ya 73, ingawa ilibidi refa Abongile Tom wa Afrika Kusini akajiridhishe kwenye VAR na la pili dakika ya 81 mara zote akimalizia pasi ya beki na Nahodha, Bakari Nondo Mwamnyeto.
  Timu hizo zitarudiana Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Pyramids ya Misri na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APIGA ZOTE MBILI YANGA YAICHAPA RIVERS 2-0 UYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top