• HABARI MPYA

  Tuesday, April 25, 2023

  YANGA WAWASILI SALAMA KUJIPANGA DAR KUJIPANGA KWA MECHI YA MARUDIANO


  KIKOSI cha Yanga SC kimerejea mapema leo Dar es Salaam kutoka Nigeria baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili Uwanja wa Venue Godswill Akpabio International mjini Uyo.
  Katika mchezo huyo mabao yote ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 73 na 81 na mara zote akimalizia pasi ya beki na Nahodha, Bakari Nondo Mwamnyeto.
  Timu hizo zitarudiana Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Pyramids ya Misri na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.
  Mafanikio makubwa ya Yanga katika michuano ya Afrika ni kufika Robo Fainali tu mara nne, mara tatu katika Ligi ya Mabingwa 1969, 1970 na 1998 na mara moja katika Kombe la Washindi 1995.

  LIGI YA MABINGWA AFRIKA:

  MWAKA 1969:
  RAUNDI YA KWANZA:
  Yanga Vs Fitaridandro (Madagascar) 4-1:0-2
  RAUNDI YA PILI:
  St. Georges (Ethiopia) Vs Yanga 0-0:0-5
  ROBO FAINALI:
  Asante Kotoko (Ghana) Vs Yanga l-l : l-l
  (Kotoko ilifuzu baada ya kupigiwa kura ya shilingi)

  MWAKA 1970:
  RAUNDI YA KWANZA:
  Yanga Vs US Fonctionnaires (Madagascar) 4-0: 2-4 
  RAUNDI YA PILI: 
  Nakuru All Stars (Kenya) Vs Yanga l-0: l-3 
  ROBO FAINALI:
  Yanga Vs Kotoko 1-1: 0-0 
  (Mechi iliunjwa dakika ya 19 ya muda wa nyongeza, na ziliporudiana katika mechi ya tatu, Kotoko ilishinda 2-0 Addis Ababa, Ethiopia)


  MWAKA 1998:
  RAUNDI YA AWALI:
  (Yanga ilifuzu moja kwa moja Raundi ya Kwanza)
  RAUNDI YA KWANZA:
  Machi 22/1998 Rayon (Rwanda) Vs Yanga  2-2 
  April 5/1998 Yanga (Dsm) Vs Rayon 1-1 
  RAUNDI YA PILI:
  Aprili 26/1998 Coffee (Ethiopia) Vs Yanga 2-2 
  Mei 9/1998  Yanga (Dsm) Vs Coffee 6-1 
  MECHI ZA KUNDI B:
  Agosti 22/98 Yanga Vs Manning Rangers 1-1 
  Sept. 6/1998 Asec  Vs Yanga 2-1 
  Sept. 20/1998 Raja Casablanca Vs Yanga 6-0 
  Okt. 10/1998 Yanga Vs Raja 3-3 
  Okt. 24/1998 Manning Rangers Vs Yanga 4-0 
  Nov. 8/1998 Yanga Vs Asec 0-3 


  KOMBE LA WASHINDI AFRIKA:

  MWAKA 1995
  RAUNDI YA KWANZA
  Vaal Reef Professionals (Af. Kusini) Vs Yanga 2-2 1-2 3-4
  RAUNDI YA PILI
  Yanga Vs Tamil Cadets Club (Mauritius) 3-1 1-1 4-2
  ROBO FAINALI
  Blackpool (Zimbabwe) Vs Yanga 2-1 2-1 4-2
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAWASILI SALAMA KUJIPANGA DAR KUJIPANGA KWA MECHI YA MARUDIANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top