• HABARI MPYA

  Friday, April 21, 2023

  MAN UNITED YATUPWA NJE EUROPA LEAGUE KWA KICHAPO CHA 3-0


  TIMU ya Manchester United impetupwa nje ya michuano ya UEFA Europa League baada ya kuchapwa mabao 3-0 na wenyeji, Sevilla usiku wa jana Uwanja wa Ramon Sanchez-Pizjuan Jijini Sevilla.
  Mabao ya Sevilla yamefungwa na mshambuliaji Mmorocco, Youssef En-Nesyri dakika ya nane na 81 na beki Mfaransa, Loïc Badé dakika ya 47 na sasa wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-2 baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza England.
  Sasa Sevilla itakutana na Juventus katika Nusu Fainali ambayo imeitoa Sporting Lisbon kwa jumla ya mabao  2-1, ikishinda 1-0 Italia na sare ya 1-1 Ureno.
  Nusu Fainali nyingine ni kati ya Roma na Bayer Leverkusen na mechi za kwanza zitapigwa Mei 11 na marudiano Mei 18.
  Bayer Leverkusen imewatoa ndugu zao wa Ujerumani kwa jumla ya mabao 5-2 wakishinda 4-1 na sare ya 1-1, wakati Roma imeitoa Feyenoord kwa jumla ya mabao 4-2 wakishinda 4-1 Italia baada ya kufungwa 1-0 Uholanzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATUPWA NJE EUROPA LEAGUE KWA KICHAPO CHA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top