• HABARI MPYA

  Saturday, April 15, 2023

  KIPA WA ZAMANI WA COSMO NA TAIFA STARS MFAUME ‘DIFU’ AFARIKI DUNIA


  ALIYEKUWA kipa wa Cosmopolitan, mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania mwaka 1967, Mohamed Mfaume ‘Difu’  (katikati) amefariki dunia Ijumaa ya Aprili 14 Jijini Dar es Salaam.
  Kipa wa timu ya taifa ya Tanzania pia kuanzia miaka ya 1960 hadi 1970 mwanzoni anatarajiwa kuzikwa leo makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.


  Mfaume Difu alikuwa kipa wa Cosmopolitan wakati inachukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania mwaka 1967, kabla ya kuifikisha Bara Fainali ya Kombe la Challenge mwaka 1970 ambako ilifungwa na Uganda.
  Mohamed Mfaume ‘Difu’ pia alikuwa mmoja kati ya wanasoka wasomi nchini ambaye alikuwa Afisa mkubwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
  Mungu ampumzishe kwa amani mlinda mlango Mohamed Mfaume ‘Difu’. Amin.


  Mohamed Mfaume ‘Difu’ wa nne kutoka kulia chini katika kikosi cha Cosmopolitan ‘The Giant Killer’ mwaka 1967.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA WA ZAMANI WA COSMO NA TAIFA STARS MFAUME ‘DIFU’ AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top